24Bongo News :
Home » » ZITTO AKANA BIFU KATI YAKE NA MBOWE

ZITTO AKANA BIFU KATI YAKE NA MBOWE



Naibu katibu mkuu wa CHADEMA Zitto Kabwe amesema hakuna mgogoro kwenye chama chake kama inavyoelezwa isipokua kuna watu wachache ambao wanataka kugombanisha viongozi wa CHADEMA.

Hii ni kauli ambayo Zitto aliitoa kwenye mkutano na wananchi Kigoma ambapo alisema kwamba CHADEMA ni wamoja isipokua ni watu wachache ndio wamekua wakieneza chokochoko.

Namkariri akisema “nataka mkae mnajua hakuna mgogoro wala tofauti ya mawazo, yani hakuna kitu ambacho mimi nasema twende hivi Mbowe anasema twende hivi isipokua kuna watu wanasema kwamba Zitto, Mbowe anakuchukia au Mbowe, Zitto anataka kukupindua....
 

Wanasema hivyo lakini mimi nataka kuwaambia watu wa Kigoma kwamba hakuna tatizo na pangekua na tatizo lolote ningeshawaambia, kuna watu wanapandikiza mbegu za chuki, kuna watu wanajaribu kufarakanisha viongozi na kujaribu kuonyesha kwamba kuna tofauti”

Zitto aliongeza kwamba: “sisi tutakua ni wajinga sana kukubali kugombanishwa, hatuwezi kukubali kuingia kwenye mgogoro kama ambao NCCR MAGEUZI waliingia kwa sababu leo CHADEMA ikianguka, ikapasuka hapatatokea chama chochote kingine cha upinzani chenye nguvu kwa miaka mingine 20 na watakaoumia ni nyie wananchi, sababu panapokua na upinzani imara wanaofaidika ni nyie, mawazo tofauti ndani ya bunge yanasikika kupitia vyama vya upinzani, mpinzani wako ni lazima atengeneze mbegu za chuki ili mgombane mfarakane”

Je wewe una maoni gani?!

Share this article :

0 comments:

KIKI POLICY


KIKI BLOG POLICY

Blog hii haina lengo la kumdharirisha mtu na pia kutoa taarifa binafsi zenye lengo la kumkwaza mtu,baadhi ya picha na habari katika blog hii hazimilikiwi na KIKI blog bali zinatoka katika vyanzo mbalimbali vya habari. Ikiwa kuna habari au picha yenye kukudharirisha basi usisite kututaharifu mapema hili iondolewe.
KARIBUNI WOTE

BANK WITH DTB 24/7

Blogger Tips and TricksLatest Tips For BloggersBlogger Tricks

WASOMAJI

Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below

Powered By Blogger Widgets

THIS BLOG IS SPONSORED BY:

THIS BLOG IS SPONSORED BY:

KUMBUKUMBU

ZILIZOVUMA

 
----
Support : Copyright © 2015. KIKI NEWS - All Rights Reserved
This blog Designed by and Modified by Joseph Richard