Mabingwa wa Afrika Mashariki na kati Yanga leo watakuwa na kibarua toka kwa mabingwa wa zamani mara mbili mfululizo wa Tanzania Bara Mtibwa sugar katiika uwanja wa taifa wakati Simba sc wakiwakabili JKT Ruvu katika uwanja wa taifa ikiwa ni mwendelezo wa ligi kuu ya vodacom.
VPL LEO FEBRUARY 2.
YANGA Vs MTIBWA SUGAR
Baada ya Yanga kupokea goli 3-0 toka kwa Mtibwa sugar katika duru la kwanza mchezo uliochezwa katika uwanja wa Jamhuri Morogoro na kupelekea kutimuliwa kwa kocha wa kikosi hicho cha jangwani na kumshuhudia Hussein Javu akiingiza mpira nyavuni mara mbili na kipa Shabani Kado kuokoa hatari lukuki katika lango lake, leo ni zamu ya yanga kulipa kisasi katika mchezo utakao chezwa uwanja wa Taifa.
Mtibwa wakitokea kufungwa goli 1 na polisi morogoro katika uwanja wake wa Manungu watakuwa na kadhi ya kurejesha imani kwa mashabiki wake baada ya kufanya vibaya katika mashindano ya mapinduzi ma kufungwa katika mchezo wao wa awali wa raundi ya pili.
Wakati wapinzani wao Yanga watakauwa na dhamira ya kuendeleza ushindi katika uwanja wa taifa na huenda kukapelekea kutangaza mapema ubingwa wa Tanzania bara.
Mchezo unahusisha Mtibwa sugar na vigogo wa soka nchini huwaga ni migumu kutabirika japo kuwa mtibwa wamekuwa na matokeo mabaya katika uwanja wa Taifa dhidi ya vigogo hao.
POLISI MORO Vs AFRICA LYON
Polisi moro walipata ushindi wao wa kwanza katika mchezo wake wa mwisho na leo katika uwanja wa Jamhuri Morogoro chini ya kocha Adolph Rishad watakuwa na kibarua cha kuendekeza ushindi huo mbele ya African lyon.
African lyon na Pelisi Moro zote zipo katika hatari ya kushuka daraja, Polisi wakiwa wamwisho katika msima wa ligi.
MGAMBO SHOOTING Vs RUVU SHOOTING, MKWAKWANI STADIUM
KESHO FEB 3
SIMBA SC Vs JKT RUVU
kesho jumapili wekundu wa msimbazi simba sc watakuwa na kibarua cha kusaka point 3 mbele ya JKT Ruvu mchezo utakaochezwa katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
Simba wakiwa wametokea kwenye ushindi wa goli 3-1 mbele ya lyon wakati JKT Ruvu wakiwa wametokea kwenye kichapo cha goli moja bila toka kwa ndugu zao ruvu shooting.
Mchezo wa raundi ya kwanza simba waliwachapa JKT Ruvu, mchezo uliochezwa katika uwanja wa taifa.
COAST UNION Vs T.PRINSONS, MKWAKWANI STADIUM
0 comments:
Post a Comment