- Loic Remy asawazisha akitokea benchi
- Diego Costa atolewa nje baada ya kupata majeruhi
- Phil Bardsley alotewa nje kwa kadi ya pili ya njano baada ya kumchezea rafu Kennedy
- Edin Hazard akosa penati ya mwisho kuifanya Stoke City kusonga mbele
Kocha Jose Mourinho ameendelea kuwa kwenye wakati mgumu kuliko kipindi chote cha maisha yake ya Soka baada ya jana akishuhudia Timu yake kutolewa nje ya mashindano ya Kombe la Ligi na kushindwa kutetea taji hilo alitotwaa msimu uliopita.
![]() |
Bardsley akitoka nje baada ya kupata kadi mbili za njano |
Safari hii timu ya Chelsea ilikuwa yenye hali na kuonekana kutawala mchezo huo mpala pale Jon Walter alipoipatia Stoke goli la kuongoza dakika ya 52 kwa shuti kali lilomshinda golia Begovic .
Loic Remy akitokea benchi aliipa Chelsea Uhai baada ya kusawazisha na kuufanya mchezo huo huende kwenye dakika 30 za nyongeza.
Katika dakika hizo za nyongeza hakuna timu iliyoweza kupata goli la kuongoza mpaka pale mshindi kuamuliwa kwa njia ya matuta.